KILA SIKU UNAWEZA...

KUWA MSHINDI KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU

1. Kabla hujampokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako, uliongoza maisha yako mwenyewe. (Isaya 53:6) 

2. Ulipompokea Yesu Kristo, Roho Mtakatifu aliingia kukaa ndani yako. (Warumi 8:9) 

3. Roho Mtakatfu humwezesha kila Mkristo kuishi maisha ya furaha. Ndio uzima ulio tele. (2 Wakorintho 3:18)

Sasa tuone jinsi...

BIBLIA INAVYOTUAMBIA HABARI ZA ROHO MTAKATIFU

Biblia inaserna:

1: Rohe Mtakatifu ni Mungu (Matendo 5:3-5) 
2. Roho Mtakatifu hukaa ndani ya kila mtu aliyempokea Kristo kuwa Mwokozi wake. (1Wakorintho 3:16) 
3. Roho Mtakatifu ni mwalimu wetu (Yohana 14:26) 
4. Roho Mtakatifu hutusaida katika udhaifu wetu (Warumi 8:26) 
5. Roho Mtakatifu anao uwezo kuliko pepo ama roho nyingine zote. (1 Yohana 4:14) 
6. Roho Mtakatifu hutuzalia matunda ya Roho katika maisha (Wagalatia 5:22, 23) 
7. Roho Mtakatifu hutupa uwezo wa kumshuhudia Kristo (Matendo 1:8)

Biblia inatuonyesha sina tatu za watu, kwanza...

1 MTU ASIYE MKRISTO  
Mtu asiye Mkrisio ni yule ambaye hajampokea Kristo kuwa Mwokozi. 

Roho Mtakatifu hakai ndani ya mtu asiye Mkristo. 

Biblia Inasems:

"Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana, kwake huyo ni upuuzi wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni." 
I Wakorintho 2:14

Tazama...
Picha hii inaonyesha namna ya

Picha hii inaonyesha namna ya

self on throne MTU ASIYE MKRISTO
chair Kiti cha enzi, yaani cha 
utawala katika maisha
self Mimi mwenyewe binafsi
cross Yesu

1. Yesu yuko nje ya maisha yake. 
2. Mtu asiye Mkristo hukaa kwenye kiti cha enzi, akitawala maisha yake mwenyewe. 
3. Huyu anahitaji kumpokea Yesu kuwa Mwokozi wake.
Mtu wa namna ya pili ni ...

2 ALIYEJAZWA (KUTAWALIWA) ROHO MTAKATIFU

Tunapompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wetu, Roho Mtakatifu huingia kukaa ndani yetu. (Warumi 8:9). Kujazwa Roho Mtakatifu, maana yake ni kumkubali Yesu kututawala na kutuongoza. 

Biblia inseleza maisha yaliyolaa Roho Mtakatifu kama hivi:

"Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi..." Wagalatia 5:22-23 
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, nata mwisho wa nchi." 
Matendo Ya Mitume 1:8

Tunapokubali Yesu atawale maisha yetu, tutapenda. kumpendeza Mungu.

Picha hii inaonyesha jinsi alivyo Mkristo aliyejazwa Roho Mtakatifu:
MKRISTO ALIYEJAA ROHO MTAKATIFU

Huyu Mkristo . . . 
*  anaye Kristo moyoni.
* anao uwezo wa Roho Mtakatifu
* huleta wengine kwa Kristo
* huomba hata kupata majibu.
* hufahamu Neno la Mungu.
* humtegemea Mungu.
* humtii Mungu
jesus on throne Malshani mwake
yatonekana haya:
* upendo
* furaha
* amani
* uvumilivu
* utu wema
* uaminifu
* upole

1. Yesu yumo maishani mwake kama Mwokozi wake. 
2. Yesu Kristo yupo katika kiti cha enzi akiongoza. 
3. Sasa yeye ni mtumishi anayemtii Yesu Kristo. 
4. Kadiri Mkristo anavyojifunza kukubali Roho Mtakatifu amwongoze, matunda ya Roho yatazidi kuonekana maishani mwake.
Lakini Mkristo asipojaa (tawaliwa) Roho Mtakatifu yeye ni...

3  MKRISTO MWENYE TABIA YA MWILINI

Mkristo mwenye tabia ya mwilini hufikiri zaldi juu ya kujipendeza kuliko kumpendeza Mungu. Hufanana na mtoto mchanga anayetaka mambo yake tu - kama watu wa dunia.

Biblia inasema haya juu ya Mkristo anayejipendeza,

"Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula: kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenda kwa jinsi ya kibinadamu?' 
1 Wakorintho 3:1-3

Sasa tazama ...

Picha hii ni ya Mkristo mwenye tabia ya mwilini 
MKRISTO MWENYE TABIA YA MWILINI

Mkristo huyu:
* hamtegemei Mungu kwa ukamilifu
* mara nyingi hatii
* havuti wengine kuja kwa Kristo
* maombi si ya maana kwake
* hapendelei sana kusoma Biblia
* mawazo yake ni maovu mara nyingi
man on throne Aweza . . . 
* kuwa na wivu
* kuwa na hatia moyoni
* kuhangaika
* kukata tamaa
* kuhukumu wengine
* kukasirika

Ujue kwamba: 
1. Yesu angali yumo maishani mwake kama Mwokozi 
2. Mwenyewe huketi kitini na kutawala maisha yake. 
3 Yesu hana utawala kamili.

Mkrlsto mwenyo table ya mwilini wakati mwlngine hutaka kumpencleza 
Mungu lakini ...

mare nyingi anataka kufanya mema asiweze ...

"Maana sijui nifanyalo; kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Ole wangu, maskini mimi! ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?" 
Warumi 7:15, 18, 24

Kutokana na hayo ...

Mkristo mwenye tabia ya mwilini hana maisha ya furaha. 
Huishi maisha ya kushindwa mara nyingi. Wakati mwingine hatendi karna Mkristo hata kidogo.

Tukumbuke tuliyoyasoma kwa kutazama tena...

ZILE AINA TATU ZA WATU

1. Mtu asiye Mkristo

2. Mkristo aliyejazwa Roho Mtakatifu

3. Mkristo mwenye tabia ya mwilini

self on throne spirtual man carnal man

Wewe ni mtu wa namna ipi? 
Ungependa kuwa Mkristo wa namna ipi? 
JE, MKRISTO WA TABIA YA MWILINI AWEZAJE KUJAZWA (KUTAWALIWA) ROHO MTAKATIFU?

TWAJAZWA (KUTAWALIWA) NA ROHO MTAKATIFU KWA IMANI 

Twapata kuwa Wakristo kwa imani katika Yesu Kristo Mwokozi wetu. Twajazwa Roho Mtakatifu kwa imani tukimtegemea Mungu na kutii neno lake. 

Unaweza kutueta hatua tatu ili kuonyesha imani yako sasa hivi.

1. WULISHE MUNGU KWAMBA UNATAKA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU. 
"Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa." Mathayo 5:6 

2. UNGAMA DHAMBI ZAKO KWA MUNGU "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zertu, na kutusafisha na udhalimu wote." I Yohana 1:9

Maana yake kuungama ni: 
a. Unakubaliana na Mungu kwamba umefanya dhambi. 
b. Unamshukuru Mungu kwa kukusamehe na kukusatisha kwa damu ya Yesu Kristo. 
c. Unaipa dhambi kisogo na kumtii Mungu, yaani kutubu.

3. JITOE KWA MUNGU

"Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hal baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki." Wanimi 6:13

Kuishi maisha yaliyojaa (kutawaliwa na) Rho Mtakatifu, hatuna budi kukbali Yesu atawale kila tutendalo.

Lazima atawale matumizi ya pesa zetu, wakati wetu wa mapumziko, kazi yetu, uhusiano wetu na jamaa na marafiki na wengine.

Je, umefahamu hatua hizi tatu? 
Je, tuzirudie tena?

UMTEGEMEE MUNGU AKUJAZE ROHO WAKE MTAKATIFU

Mungu atakujaza (kukutawala na kukuwezesha) na Roho wake 
Mtakatifu kama ukimtegemea akufanyie hivyo. 

Kuna maneno mawili muhimu kukumbuka

1. UTII AGIZO LAKE KUJAZWA 
"Msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho." Waefeso 5:18 

2. TEGEMEA AHADI YAKE KUKUJAZA 
"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake,ya kuwa,tukiomba kitu,sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba." I Yohana 5:14-15

Hata sasa...

UNAWEZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU KWA IMANI

Njia moja kuonyesha imani yako ni kwa maombi.

UNAWEZA KUOMBA HIVI:

 "Bwana Yesu, ninakuhitaji kuongoza maisha yangu. Nimekuwa nikijitawala maisha yangu mwenyewe. Sasa nakubailana nawe kwarnba hil ni dhambi. Dhambi hil ninaipa kisogo na kujitoa kwako kukutil. Asante kwamba umenisamehe. Sasa natil agizo lako na kukuamini unijaze na Roho Mtakatifu. Asante sana kwa kunijaza kame ulivyoahidi!' Amin.

Je, utapencla kumwomba Mungu akujaze na kukutawala na kuwezesha maisha yako? 

Je, ungependa kuomba sala hii sasa?

KWA IMANI UNAWEZA KUJUA KWAMBA UMEJAA (KUTAWALIWA NA) ROHO MTAKATIFU

Je, ulijitayarisha kama tulivyoeleza katika kurasa 12 hadi 14? 
Je, ulimtegemea Mungu kwa imani akujaze na Roho Mtakatifu? 
Picha hii yaonyeshajinsi Ukweli wa Biblia, na Imani, na hali ya moyo (maoni) zinavyolingana katika maisha yako ya Kikristo.

truck

1. Mungu anakuagiza kwmba ujazwe Roho Mtakatifu. Ni ahadi yake kukujibu unapoomba kulingana na mapenzi yake. 
2. Unapokea uwezo wa Mungu ukitegemea kwamba atatimiza ahadi yake. 
3. Unapotegemea Mungu kukujaza, atakupa nguvu ya kuishi maisha matakatitu na kwa kuwashuhudia wengine wamjue Kristo. 
4. Usisahau, unamtegemea Mungu kukujaza, na hutegemei hali ya moyo na mawazo. Mungu hatakosa kutimiza ahadi yake kukujaza. Mungu si mwongo. 
5. Kwa sababu Mungu ni mwaminifu, sasa unaweza kumshukuru kwa kukujaza, Roho Mtakatifu, hata kama huoni tofauti yo yote.

UNAWEZA KUENDELEA KUJAZWA (KUTAWALIWA) NA ROHO MTAKATIFU

Kama ukifanya dhambi tena kwa kuongoza maisha yako mwenyewe, inakupasa kufanya mambo mawili. 

1 . Ungama dhambi yako kwa Mungu. Yeye atakusamehe na kukusafisha tena, (I Yohana 1:9). Uipe dhambi hii kisogo na kumtii Mungu. 

2. Unahitaji kujazwa (kutawaliwa na kupata nguvu) kwa Roho Mtakatifu tena. Mwombe Yesu Kristo kutawala maisha yako. Utii AGIZO la Mungu kujazwa Roho Mtakatifu. Tegemea AHADI ya Mungu kukujaza. Waefeso 5:18, 1 Yohana 5:14-15.

Fuata njia hizi mbili kila mara Roho Mtakatlfu anapokuonyesha dhambi maishani mwako. Nawe utakuwa na maisha ya furaha na kuzaa matunda ya kiroho. 

UMTEGEMEE ROHO MTAKATIFU AENDELEE KUKUJAZA (KUKUTAWALA) HIVYO. NDIPO YESU KRISTO ATAKUWA KATIKA KITI CHA ENZI CHA MAISHA YAKO KILA SIKU.

Unaweza kujua kwamba ...

WAKATI ROHO MTAKATIFU ANAPOKUONGOZA NA KUKUTAWALA MAISHA YAKO:

1. Matunda ya Roho Mtakatifu yatazidi kuonekana katika maisha yako (Wagalatia 5:22-23). 

2. Maombi yako yatazidi kusikika (Yakobo 5:6). 

3. Utazidi kufahamu Biblia (2 Timotheo 3:16). 

4. Utakuwa na uwezo wa Mungu kumshuhudia. (Matendo 1:8). 

5. Utakuwa na uwezo wa Mungu kushinda majaribu na dhambi. (I Kor. 10: 13). 

6. Utamwamini Mungu na ahadi zake (2 Petro 1:3-11). 

7. Utaendelea kuishi maisha ya Mkristo aliyeujazwa Roho Mtakatifu kwa imani 
(Waebrania 11:6; 1 Yohana 5:1-5) 

8. Utakuwa na ushind juu ya pepo wabaya (mashetani). (1 Yohana 4:1-4).

Ni jambo muhimu...

KWENDA KANISANI 

Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25) 

Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikilundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kaishi maisha ya kikristo peke yako. 

Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani. 

Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa. 

Kama kweli hii imekusaidia ...